1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Taliban wakwamisha maendeleo ya ujenzi mpya.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClK

Kiongozi wa ujumbe wa hivi sasa wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ameonya kuwa Afghanistan iko njia panda na wapiganaji wa Taliban wanaleta kitisho kikubwa katika ujenzi mpya wa nchi hiyo. Balozi wa Japan katika umoja wa mataifa Kenzo Oshima amesema hali ya kutokuwa na usalama inaendelea kuwako katika maeneo ya kusini na mashariki ya Afghanistan . Na licha ya ongezeko la ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo pamoja na ujenzi mpya unaoongozwa na jumuiya ya kimataifa, uzalishaji wa bangi na ulaji rushwa ni mkubwa sana, na kuwaacha Wafghan wakiwa hawaridhishwi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Pakistan Khursheed Kasuri , ambaye anaitembelea Afghanistan , ameambiwa na rais Hamid Karzai kuwa uvumilivu wa raia wa nchi hiyo unakaribia kutoweka kwa sababu ya mipaka kutokuwa salama. Afghanistan imekuwa ikidai kuwa Pakistan inahifadhi wapiganaji wa Taliban.