1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Taliban waweka muda mwingine wa mwisho.

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdr

Nchini Afghanistan , wapiganaji wa Taliban wameweka muda mwingine wa mwisho kwa ajili ya majadiliano yatakayohusu hali ya baadaye ya mateka 22 waliobaki wa Korea ya kusini.

Wapiganaji hao wenye imani kali wametishia kuanza kuwauwa mateka wao kuanzia mchana leo Jumatatu iwapo serikali haitawaachia waasi wanane walioko kifungoni.

Maafisa hawajatoa maelezo zaidi kuhusiana na mikutano ya faragha , lakini hadi sasa wameondoa uwezekano wa kuwatoa wafungwa hao kwa kubadilishana na mateka. Wapiganaji tayari wamekwisha muua mateka mmoja.