1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Ufaransa yapewa wiki moja kuyaondoa majeshi yake.

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8d

Wapiganaji wa Taliban wanaowashikilia wafanyakazi wawili wa kutoa misaada raia wa Ufaransa kusini mwa Afghanistan wameipa Ufaransa wiki moja kuyaondoa majeshi yake kutoka nchini humo ili kunusuru maisha ya mateka hao.

Katika taarifa iliyotumwa katika tovuti ya taliban , wapiganaji hao wamesema hatua za haraka zitachukuliwa dhidi ya wafanyakazi hao wa kutoa misaada iwapo serikali ya Ufaransa itakataa madai yao.

Raia hao wa Ufaransa walikamatwa mapema mwezi huu katika jimbo la kusini magharibi la Nimroz.