1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Waandishi wa DW wauwawa.

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD50

Waandishi wawili wa kujitegemea wa shirika la utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle wameuwawa nchini Afghanistan.

Watu wenye silaha wasiotambulika wamewapiga risasi Karin Fischer na fundi wake Christian Struwe katika hema lao mapema jana Jumamosi asubuhi.

Waandishi hao wawili walikuwa wakifanya utafiti kwa ajili ya kutayarisha makala maalum katika jimbo la Baghlan, kiasi cha kilometa 120 kaskazini ya mji mkuu wa Afghanistan wa Kabul.

Mkurugenzi wa Deutsche Welle Erik Bettermann ametoa rambi rambi zake kwa familia ya Fischer na Struwe na kusifu kazi waliokuwa wakifanya.

Maafisa wa Afghanistan wamekataa kuwa tukio hilo ni la uporaji tu. Hili ni tukio la kwanza la kuuwawa kwa waandishi wa habari nchini Afghanistan tangu mwaka 2001.