1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Wajerumani watatu wauwawa Afghanistan

16 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYn

Bomu lililotegwa lililotegwa barabarani nje kidogo ya kusini mashariki mwa mji wa Kabul nchini Afghanistan limeuwa raia watatu wa Ujerumani.

Wizara ya mambo ya ndani mjini Berlin imesema watu hao watatu ni maafisa wa polisi wa Ujerumani waliowekwa nchini Afghanistan kuulinda ubalozi wa Ujerumani.Kundi la Taliban limedai kuhusika na mripuko huo.Mjerumani wa nne alijeruhiwa katika shambulio hilo ambalo limepoteza idadi kubwa ya maisha kwa Ujerumani kuwahi kushuhudiwa tokea mwezi wa Mei.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amelilaani shambulio hilo na kwa niaba ya serikali ya shirikisho ya Jamhuri ya Ujerumani na kwa niaba yake mwenyewe binafsia ametuma rambi rambi kwa ndugu za wahanga na kuwa pamoja nao katika kipindi hiki cha maombolezo.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amesema ameshtushwa na kusikitishwa na vifo hivyo.

Hata hivyo viongozi wa Ujerumani wamesema kwamba shambulio hilo halitowalazimisha kubadili sera yao ya kuunga mkono serikali ya Afghanistan.