1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanadiplomasia wa Korea Kusini wakutana na Taliban

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVB

Wanadiplomasia wa Korea Ksuni watakutana na wanamgambo wa kundi la Taliban mjini Ghazni mashariki mwa Afghanistan hii leo kujadili hatima ya mateka 19 wa Korea Kusini.

Zimepita wiki mbili tangu wapatanishi walipokutana ana kwa ana na watekaji nyara wanaowazuilia mateka hao.

Duru za kidiplomasia zinasema mazungumzo kati ya Taliban na maafisa wa Korea Kusini yamefikia ngazi muhimu huku wanamgambo hao wakiendelea kudai wafungwa wao waachiwe huru kutoka magerezani, kabla kuwaachia mateka.

Mateka 23 wa Korea Kusini walitekwa nyara na wanamgambo wa Taliban mnamo tarehe 19 mwezi uliopita wakati walipokuwa wakisafiri kutoka mji mkuu Kabul kwenda Kandahar.

Mateka wawili wakiume waliuwawa baada ya serikali ya Afghanistan kukataa kutimiza masharti ya Taliban.