1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Wanajeshi saba wauwawa katika ajali ya helikopta.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwQ

Msemaji wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan amesema kuwa wanajeshi saba wa jeshi la NATO wameuwawa katika ajali ya helikopta.

Msemaji wa kundi la Taliban hapo mapema alidai kuhusika na kuungushwa kwa helikopta hiyo ambayo ilianguka katika wilaya ya Kajaki katika jimbo la Heimand.

Jeshi la ISAF lenye wanajeshi kutoka mataifa 37 halikutoa uraia wa wanajeshi hao hadi pale nchi zao zitakapofanya hivyo, licha ya kwamba afisa wa Marekani alieleza kuwa watano kati ya waliouwawa ni Wamarekani.

Vifo hivyo vya sasa vinaongeza idadi ya wanajeshi wa kigeni waliouwawa nchini Afghanistan mwaka huu kufikia 73.