1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanajeshi wanane wa Marekani wauwawa

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQt

Jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani nchini Afghanistan limesema wanajeshi wanane wa Marekani wameuwawa na wengine 14 kujeruhiwa wakati helikopta yao ilipoanguka katika eneo la kusini mashriki linalokabiliwa na upinzani mkali. Taarifa ya jeshi hilo imesema helikopta hiyo ilianguka kwa sababu ya kupoteza umeme kwa ghafla.

Helikopta hiyo ilianguka jana asubuhi katka mkoa wa Zabul, yapata kilomita 250 kusini magharibi mwa mji mkuu Kabul.

Hapo awali wanamgambo wa kundi la Taliban walitangaza waliitungua helikopta hiyo kutumia roketi.