1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanajeshi wengine wa Marekani wauawa nchini Afghanistani

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6a

Duru za majeshi ya Marekani yaliyoko nchini Afghanistani zinasema kuwa wanajeshi wawili wa Marekani na mwanajeshi mmoja wa Afghanistani waliuawa katika mapigano na waasi wa kitalibani katika eneo la mashariki ya nchi. Duru hizo zimezidi kusema kuwa wanajeshi wengine watatu wa Marekani wamejeruhiwa katika mapigano ya jana usiku katika wilaya ya Pech mkoa wa Kunar mashariki ya nchi.

Mapema jana pia, mtu aliyekuwa na bomu alijilipua karibu na msafara wa wanajeshi wa NATO katika mji mkuu Kabul na kuwajeruhi wanajeshi watatu na raia watatu vile vile.