1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanamgambo 12 wameuawa Afghanistan

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBwB

Wanajeshi wa Afghanistan na wa shirika la kujihami la nchi za magharibi-NATO wamewaua si chini ya watu 12 walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Taliban.Kwa mujibu wa maafisa wa Kiafghanistan, wengi wengine walijeruhiwa pia.Mashambulio hayo yalitokea katika wilaya ya Helmand,kusini mwa Afghanistan.Wakati huo huo maafisa wa NATO wamesema,helikopta iliyoanguka na kusababisha vifo vya wanajeshi wake 7 huenda ikawa ilipigwa na adui.Helikopta hiyo ilianguka Kajaki katika wilaya ya Helmand.Miongoni mwa wanajeshi waliofariki katika ajali hiyo,5 ni Wamarekani.