1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanamgambo wa Taliban wabadili mbinu za mashambulizi

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqI

Maafisa wa usalama nchini Afghanistan wamesema, wanamgambo wa Kitaliban wamefanya mashambulizi ya mfululizo,katika eneo la milimani la Uruzgan, kusini mwa nchi.Hadi watu 60 wameuawa katika mapigano ya siku nne zilizopita.Mashambulio ya waasi kusini mwa nchi yadhihirisha kuwa ni makubwa kabisa kupata kufanywa na wapiganaji wa Taliban mwaka huu.Vile vile mashambulizi hayo yanatumia mbinu tofauti kulinganishwa na mashambulizi ya bomu ya kujitolea muhanga,kando ya barabara.Nchini Afghanistan,hadi hivi sasa, kama watu 2,400 wameuawa katika mapigano ya mwaka huu.