1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanamgambo wa Taliban wapata pigo Afghanistan

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwG

Majeshi ya Afghanistan yakishirikiana na wanajeshi wa muungano wa NATO wamewaua kiasi wanamgambo kumi na wawili wa Taliban kwenye makabiliano katika mkoa wa Helmand kusini mwa nchi hiyo.

Maafisa wa serikali ya Afghanistan wamesema wanamgambo kadha walijeruhiwa kwenye mashambulio ya ndege za NATO.

Wakati huo huo maafisa wa NATO wamesema huenda ndege ya helikopta iliyoanguka na kusababisha vifo vya wanajeshi wake saba iliangushwa na maadui.

Helikopta hiyo ilianguka katika wilaya ya Kajaki, mkoani Helmand.

Wanajeshi watano miongoni mwa hao waliofariki walikuwa wamarekani.