1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanamgambo wa Taliban wauawa Afghanistan

7 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBl7

Zaidi ya wapiganaji 30 wa Taliban wameuawa kusini mwa Afghanistan.Msemaji wa majeshi yanayoongozwa na Marekani nchini Afghanistan akieleza habari hiyo aliongezea kuwa mapigano yalianzishwa na wanamgambo.Amesema,polisi na wanajeshi wa Kiafghanistan walishambuliwa kwa risasi na gruneti zilizorushwa kwa makombora.Wakati huo huo wakazi wa vijijini katika wilaya ya Kunar, mashariki mwa Afghanistan wanasema,raia 35 wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na vikosi vya kimataifa.Mashambulizi hayo yamethibitishwa na msemaji wa vikosi vinavyoongozwa na NATO,lakini amesema,hakuna ripoti kuhusu wahanga wa kiraia.Majira haya ya joto,mapigano ya kukomesha uasi wa Wataliban wanaoungwa mkono na Al-Qaeda,yameimarishwa katika kila pembe ya Afghanistan.