1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Wapiganaji waipa serikali muda zaidi.

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeZ

Wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan wamesema kuwa wataipa serikali muda zaidi ili kuruhusu mjumbe kutoka Korea ya kusini kujiunga na mazungumzo kwa ajili ya kuwaacha huru mateka 22 wanaowashikilia.

Mjumbe wa Korea ya kusini anatarajiwa kuwasili mjini Kabul ili kufanya mazungumzo ya haraka na rais Hamid Karzai wa Afghanistan pamoja na majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani kufuatia wito wa haraka uliotolewa na mmoja wa mateka hao wafanyakazi wa kutoa misaada wa kanisa ili kusaidiwa.

Wapiganaji, hata hivyo , wamerudia kitisho chao cha kuwauwa wafanyakazi hao iwapo serikali ya Afghanistan haitawaachia wafungwa wanane waasi. Kundi la Taliban hapo awali liliweka muda wa mwisho jana mchana kupanga kuwaachia wafanyakazi hao wa kutoa misaada kutoka Korea ya kusini ambao hivi sasa wako katika siku yao ya tisa wakiwa mateka. Kiongozi wa kundi hilo tayari amekwisha uwawa.