1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Watu tisa wauwawa kwenye maandamano

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxG

Watu tisa wameuwawa na wengine 32 wakajeruhiwa kwenye maandamano makubwa yaliyofanyika katika mkoa wa Jowzjan kaskazini mwa Afghanistan.

Maandamano hayo ya kumpinga gavana wa jimbo hilo yalikumbwa na machafuko ambapo polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiwarushia mawe katika mji mkuu wa jimbo hilo, Shiberghan.

Msemaji wa polisi amesema polisi walifyatua risasi angani kuwatawanya waandamanaji wa mbabe wa mbari ya Uzbek, Abdul Rashid Dotstam. Madaktari wanasema majeraha mengi yamesababishwa na risasi.

Hapo awali waafghanistan waliuwawa mjini Kundus na mwengine mmoja kujerihiwa katika shambulio la bomu lililofanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha kaskazini mwa Afghanistan.

Shambulio hilo liliwalenga washauri wa polisi ya Afghanistan kutoka Marekani walio katika mji wa kaskazini wa Kundus.

Kundi la wanamgambo wa Taliban limesema limefanya shambulio hilo.