1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul.Kiasi cha raia 50 watajwakuuwawa katika mapigano ya wiki hii huko Afghanistan.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz7

Maafisa nchini Afghanistan wamesema kwamba, kiasi cha raia 50 wameuwawa kufuatia mashambulio ya NATO huko kusini mwa Afghanistan mapema wiki hii.

Mmoja wa maafisa wa baraza la mji amesema, hadi raia 80 wameuwawa katika jimbo la Kandahar siku ya Jumanne.

NATO imesema imepokea taarifa za kuuwawa kwa watuhumiwa 45 wa kitaliban huko Kandahar wakati wa mapigano.