1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Kiongozi wa Taliban auwawa

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2N

Kikosi cha ISAF kinachoongoza wanajeshi wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO,kimethibitisha kuuwawa kwa kamanda mkuu wa wapiganaji wa kitaliban nchini Afghanstan Mullah Dadullah.

Dadullah ambaye ni miongoni mwa viongozi wa juu wa kundi la Taliban aliuwawa kwenye opresheni iliyofanyika kwenye mkoa wa Helmand.

Kikosi cha ISAF kimetaja kuuwawa kwa Dadullah kuwa kipigo kikubwa kwa wapiganaji wa Taliban nchini humo.

Dadulla ametajwa kuwa mpiganaji jahil wa kundi la Taliban ambaye amepigana na vikosi vya kisovieti katika miaka ya themanini na alihusishwa na mauaji kadhaa kabla na baada ya kuanguka kwa utawala wa Taliban mwaka 2001.