1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Madawa yadondoshwa kwa ajili ya mateka wa Korea Kusini

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbh

Madakatari nchini Afghanistan wamewasilisha madawa kwa ajili ya mateka 21 wa Korea Kusini wanaozuiliwa na na kundi la Taliban kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Madaktari hao wamedondosha madawa hayo katika eneo la Ghazni linalomilikiwa na waasi.

Kundi la Taliban limetowa taarifa kuwa wengi kati ya mateka hao wa Korea Kusini wanauguwa wawili wakiwa katika hali mahututi. Kundi la Taliban limetishia kuwauwa mateka zaidi kutokana na kutokuwepo maendeleo yoyote katika majadiliano kuhusu mateka hao. Kundi hilo linataka serikali iwaachie huru wafungwa wa kundi hilo la waasi kutoka gerezani.

Serikali mjini Kabul hadi sasa imekataa kukidhi madai ya kundi la Taliban serikali hiyo inasema kukubali madai ya waasi ni sawa na kushawishi vitendo zaidi vya utekaji nyara. Rais Hamid Karzai ambae amewasili nchini Marekani kwa mazungumzo na rais Bush amesema serikali yake itafanya kila jitihada ili mateka hao waachiwe huru.

Viongozi hao wanatarajiwa kujadili hali ya usalama inayozidi kudidimia nchini Afghanistan na vitisho vya wapiganaji wenye msimamo mkali wanaojificha nchini Pakistan.

Wakati huo huo kamati ya dharura hapa nchini Ujerumani inaendelea na juhudi za kusaka uhuru wa mhandisi wa Kijerumani aliyetekwa nyara nchini Afghanistan.