1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:"Mataliban " zaidi wauliwa

22 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Di

Watu wasiopungua 20 waliotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kitaliban wameuawa katika mapigano na majeshi yanayoongozwa na NATO nchini Afghanistan.Raia 11 pia walijeruhiwa kutokana na mapigano hayo yaliyotokea mashariki mwa nchi.

Maafisa wa NATO wamewalaumu mataliban kwa kuwatumia raia kama ngao katika mapambano. Habari zaidi zinasema watu wengine zaidi ya 30 waliotuhumiwa kuwa mataliban pia waliuliwa katika mapambano na majeshi ya Afghanistan yaliyoshirikiana na askari wa NATO kusini mwa Afghanistan.