1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:raia wengine wauliwa na wanajeshi

7 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hl

Askari wa jeshi la kimataifa nchini Afghanistan wamewaua raia watatu wa nchi hiyo.

Habari zinasema askari hayo walifyatua risasi baada ya watu hao kupinga amri ya kusimama kwenye vituo vya ukaguzi.

Mkasa kama huo ulitokea jana vilevile ambapo askari waliwaua raia wawili waliokuwamo ndani ya lori ambalo halikusimama kwenye kituo cha udhibiti licha ya kuamrishwa kufanya hivyo.

Msemaji wa jeshi la kimataifa nchini Aghanistan ameeleza masikito juu ya matukio hayo na amesema kuwa uchunguzi utafanyika.