1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Taliban wadai kuhusika na shambulizi la kujitoa mhanga

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKq

Kundi la Taliban limedai kuhusika na shambulizi la kujitoa mhanga lililoua watu 12 wakiwemo askari polisi wa Afghanistan hata hivyo baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa huenda idadi ya waliyokufa ikawa kubwa zaidi.

Maafisa wa polisi wamesema kuwa watu wengine 15 walijeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo ni la pili kutokea mjini Kabul katika kipindi cha siku nne zilizopita.

Msemaji wa kundi la Taliban amesema kuwa wanaharakati wa kiislam wanaopigana dhidi ya serikali na kuyaondoa majeshi ya kigeni nchini humo wanahusika na shambulizi hilo.