1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Taliban wakataa mazungumzo na rais Karzai

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLO

Rais Hamid Karzai wa Afghanstan amesema yuko tayari kukutana kwa mazungumzo na viongozi wakuu wawili wa wapiganaji katika juhudi za kuleta amani nchini mwake.

Rais Karzai ametoa changamoto kwa kiongozi wa kundi la Taliban Mulla Mohammed Omar na Gulbuddin Hekmatyar wa kundi la itikadi kali la Hezb-i-islami kushiriki katika uchaguzi mkuu.

Aidha amesema atawajumuisha katika serikali yake kwa sharti kwamba watajiepusha na kuhusika katika mashambulio.Hata hivyo kundi la Taliban leo hii limekataa mazungumzo yoyote na rais Karzai na badala yake limetaka wanajeshi wote wakigeni waondoke Afghanstan.Matamshi ya rais Karzai ya kutaka mazungumzo na wanamgambo yamekuja saa chache baada ya mshambuliji wa kujitoa muhanga kuua watu kiasi cha 27 na kuwajeruhi wengine wengi katika mji mkuu Kabul.Amelaani shambulio hilo akisema wanaobeba dhamana ya tukio hilo ni maadui wau tu.Wanamgambo wakitaliban wamedai kuhusika na shambulio hilo lililolenga basi la wanajeshi.