1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL.Waasi kumi na watano wauwawa

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0C

Majeshi ya muungano wa NATO yamewauwa waasi 15 kusini mwa Afghanistan baada ya waasi hao kuushambulia msafara wa kijeshi kwa bunduki na roketi.

Mashambulio hayo yametokea katika jimbo la Zabul hata ingawa hakuna habari zaidi zilizotolewa.

Takriban wanajeshi 31,000 wa muungano wa kijeshi wa NATO, ISAF wako nchini Afghanistan kuisaidia serikali ya nchi hiyo kupambana na wapiganaji wa kundi la Taliban ili kufanikisha ujenzi wa nchi hiyo.