1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadi ya Buluu

20 Novemba 2008

Kadi ya buluu kumwezesha mgeni mwenye ujuzi na ufundi kuhamia nchi ya Umoja wa Ulaya kuidhinishwa leo Strassbourg:

https://p.dw.com/p/FylK

Bunge la Umoja wa Ulaya, leo linapiga kura kuidhinisha matumizi ya "Blue Card"-utoaji wa kadi za rangi bluu kuwaruhusu wahamiaji kuhamia nchi za Umoja huo wakiwa na ujuzi na ufundi unaohitajika katika nchi hizo.kanuni zitakazoamuliwa zitapaswa kutekelezwa mnamo miaka 2 ijayo.

Ramadhan Ali na ripoti zaidi:

Hapo kabla ikionekana kana kwamba wabunge wa Ulaya hawakutarajia tena "Kadi ya Buluu" kuja kutumika. Mbunge Manfred Weber anasema:

"Hapa kuna maswali ya mila na kufungua milango wazi kwa uhamiaji."

Tunataka kuwa na wahamiaji wa aina hiyo tena bora leo kabla ya kesho.Weber ni mbunge kutoka chama cha CSU cha mkoa wa Bavaria nchini Ujerumani ambacho si miongoni mwa vyama vinavyolilia sana mchanganyiko wa makabila na mila mbali mbali humu nchini.Muwakilishi wa chama hicho katika Bunge hilo la Ulaya anafuata mkondo wa upepo unakovuma barani ulaya wakati huu:

Mnamo miaka 20 ijayo imekisiwa kuwa katika nchi za Umoja wa Ulaya kutakosekana wataalamu hadi milioni 20 wa fani mbali mbali .Kuziba pengo hilo,inapangwa sasa kufungua mlango kwa wahamiaji kutoka ngambo nje ya nchi za Umoja wa Ulaya wenye ujuzi na elimu maalumu. Hivyo ndivyo inavyosemekana tangu mjini Brussels,makao makuu ya UU hata Strassbourg, kwenye Bunge la Umoja huo.

Bunge la Ulaya na serikali za nchi zote 27 zanachama baada ya majadiliano marefu zimeafikiana sasa kutoa "kadi ya buluu" na kuanza kazi ikikawia kabisa miaka 2 ijayo.

Baadae kila kitu kitarahisika kwa muujibu asemavyo mbunge wa Ulaya kutoka chama cha SPD cha Ujerumani Bw.Wolfgang Kreissl-Dorfer-wote watanufaika:

"Kampuni linalomhitaji bingwa haraka kwa kazi, laweza kumuajiri hata mgeni kutoka nje ya UU.Mtu mwenye ujuzi wa hali ya ujuu na anaetaka kuhamia Ulaya ataweza hapo kuajiriwa.Bila shaka kwa kurahisishwa sheria za kuingia na kutoka nchini,mtu huyo atakuwa na uhuu wa kurejea kwao na maarifa mapya aliojipatia huku akastawisha uchumi huko kwao.Nionavyo mimi, hali hii ni nafuu mara tatu."

Nani atakuwa na dhamana ya kutoa kadi hizo za buluu-je, Idara inayowahudumia wahamiaji wa kigeni,Idara za kazi au Taasisi nyengine yoyote,haijulikani kwa sasa na ni jukumu lililoachiwa serikali ya kila nchi kuamua.Wazi ni kuwa masilahi ya Ulaya yanahifadhiwa katika kinyanganyiro cha kuania wataalamu na nafasi za kazi.

Mbunge wa Ulaya Weber anaongeza:

"Endapo kuna raia wa nchi za Ulaya wenye ujuzi na ufundi unaotakikana,basi kwanza wapewe wao kabla wale wenye kadi za bluu...."

Kadi za buluu (Blue Cards) kwa wataalamu au mafundi wa ujuzi wa juu kutoka nchi zisizo za Umoja wa Ulaya ni mchangamnyiko wa rfuhusa ya kukaa nchini na ya kufanya kazi .Itatolewa kwa kipindi cha miaka 3 na itaweza kurefushwa kwa kipindi cha miaka 2 zaidi.

Fundi-mitambo kutoka Sri Lanka au bingwa wa komputa kutoka Indonesia,lazima aoneshe analipwa mshahara wa juu zaidi katika nchi aliyohamia kufanya kazi na kuishi kuliko wa wastani.Iwapo ni mkubwa mara moja na nusu zaidi au hata mara mbili zaidi ya ule wa nyumbani, ni jukumu la nchi mwenyeji kuamua.

Kwa njia hii, Umoja wa Ulaya na hasa serikali ya Ujerumani, unahisi umewaridhia hasa wale ambao hawakuonesha ushabiki wa "kadi za buluu" na walipendelea zaidi kurahisisha uhamiaji nchini mwao.Licha ya hivyo, kadi ya buluu itatumika pia nchini Ujerumani na leo hii itaamuliwa kabisa na Bunge la Ulaya mjini Strassbourg na mwezi ujao wa Desemba Baraza la mawaziri la Umoja wa Ulya litatoa idhini yao rasmi na kabla kumalizika miaka 2 itaanza kutumika.