1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadinali Nasrallah awataka wabunge wamchague rais mpya

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CT3A

Kadinali Nasrallah Sfeir wa jamii ya Maronite inayotoa marais wa Lebanon, amewatolea mwito wanasiasa wakubaliane kuhusu rais mpya ili kuzuia machafuko nchini Lebanon.

Katika mahubiri yake kwenye ibada ya jana Jumapili, Nasrallah alisema Lebanon iko katika kipindi cha mpito kinachoweza kuilekeza katika uthabiti au machafuko na kuwataka wahusika wote wawe waaminifu na waonyeshe uzalendo.

Hapo kabla chama cha Hezbollah kinachoungwa mkono na Syria, kilipinga vikali uamuzi wa serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora inayoungwa mkono na nchi za magharibi, kuchukua madaraka ya kuiongoza Lebanon baada ya rais Emile Lahoud kuondoka bila mrithi kufuatia muhula wake kumalizika.

Ingawa wabunge wameahidi kufikia makubaliano kuhusu rais mpya katika kikao cha bunge kitakachofanyika Ijumaa ijayo, hakujakuwa na ufanisi wa maana kufikia sasa.