1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KALITI:Wanaharakat 38 washtakiwa kukiuka katiba

11 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsj

Wanaharakati 38 wa upinzani nchini Ethiopia wameshtakiwa kwa kukiuka katiba ya nchi.kesi hiyo ilifunguliwa baada ya ghasia kutokea katika uchaguzi uliosababisha utata mwaka 2005.Wanachama 38 wa chama cha Coalition for Union and Democracy,CUD walikataa kutambua kesi hiyo na kuamua kutojitetea mahakamani.

Watu 22 walipatikana na hatia ya kuzuia taratibu za katiba kuendelea..watano wengine kupanga na kufanya vitendo vya ghasia dhidi ya serikali na 10 waliosalia walipatikana na hatia ya kuhatarisha usalama wa kitaifa.Hukumu hizo zitatolewa mwezi ujao tarehe 8.

Hukumu ya washtakiwa wengine 12 waliowakilishwa mahakamani inasubiriwa kutolewa tarehe 18 mwezi huu.

Serikali ya Ethiopia imekuwa ikilaumu chama cha CUD kwa kusababisha ghasia na kupanga njama ya kupindua serikali tangu uchaguzi wa mwezi mei mwaka 2005.Vyama vya upinzani unadai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na ila.Yapata watu 193 walipoteza maisha yao katika ghasia zilizotokea mjini Addis Ababa katika uchaguzi mwezi Juni na Novemba mwaka 2005.