1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Iraq, ataka jeshi la nchi hiyo, kupewa muda nchini Iraq.

Nyanza, Halima9 Aprili 2008

Kamanda wa Jeshi la Marekani nchini Iraq, Jenerali David Petraeus ametoa wito wa kuahirishwa kuondolewa kwa jeshi hilo nchini humo, angalau siku 45 baada ya mwezi wa saba akionya mafaninikio yaliyopata bado si imara.

https://p.dw.com/p/Deg6
Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Marekani nchini Iraq, David Petraeus.Picha: AP

Akitoa taarifa ya kwanza katika kipindi cha miezi saba kwa bunge la nchi hiyo, Kamanda huyo wa Jeshi la Marekani nchini Iraq pia ameilaumu Iran kwa kujaribu kuchochea ghasia.

Amependekeza kwa wabunge hao, kwamba endapo wanajeshi wa mwisho kati wanajeshi wa ziada elfu 30 walioopelekwa nchini Iraq mwaka uliopita, wanaopaswa kuondoka mwezi Julai, waongezewe muda zaidi kama siku 45 ili kuweza kuangalia hali ya mambo ilivyo nchini humo.

Hata hivyo kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Iraq, wabunge kupitia chama cha siasa cha Democratik wamedai kuwa Jenerali huyo mkuu wa jeshi la Marekani nchini Iraq alikuwa akitaka kupewa ruhusa ili majeshi, yakae huko kwa muda zaidi katika kuendeleza vita hivyo visivyopendwa ambavyo tayari vimesababisha mauaji ya zaidi ya wa Marekani elfu 4, wakati huu ambao vita hivyo vinaingia katika mwaka wake wa sita.

Kiongozi huyo wa Kijeshi wa Marekani nchini Iraq ambaye alikuwa amefuatana na Balozi wa Marekani nchini Iraq Ryan Crocker kutoa taarifa yao hiyo kwa bunge ameonya kuwa wakati hali ya usalama ikiwa inaimarika katika maeneo mengi na majeshi ya iraq yakiwa yanaendelea kuchukua majukumu zaidi hali nchini Iraq bado ni ngumu na yenye kuleta changamoto.

Ameongeza kusema kuwa vikosi vya marekani vilivyoivamia Iraq Machi, 2003 huenda vikakabiliana na mashambaulizi ya wapiganaji wa Al-qaida nchini Iraq ama mapigano zaidi na wanamgambo wa kishia kama vile makundi yanayoongozwa na kiongozi mwenye msimamo mkali Mogtada Al Sadr.

Katika hatua nyingine, wagombea watatu wa kiti cha Urais nchini Marekani, pia walipata nafasi ya kumuuliza maswali kamanda huyo mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, pamoja na Balozi wa Marekani nchini humo, ambapo Mgombea kupitia chama cha Democratic Barack Obama aliitaka nchi yake kuongeza shinikizo kwa Wairaq kutatua tofauti zao.

Aidha, ametoa wito wa kuchukuliwa juhudi zaidi za kidiplomasia ikiwemo mazungumzo na Iran, ili kusaidia kuimarisha utulivu nchini Iraq.

Kwa upande wake, Seneta Hilary Clinton ambaye anapambana na Barack Obama kuwania nafasi hiyo ya Urais kupitia chama kimoja, amesema kwa sasa anafikiri ni wakati wa kuanza kuondoa majeshi yao nchini humo na kutatua matatizo mengine kuanza kujenga upya jeshi pamoja na kulenga changamoto nyingine kama vile kuhusiana na Afghanistan, makundi ya kigaidi dunian.'

Lakini kwa upande wake, mgombea Urais kupitia chama cha Republican John McCain, amepinga kuondolewa kwa majeshi hayo kwa ksema kuwa Marekania haikop tayari kushindwa katika vita hivyo.

Ameongeza kuwa anatarajia mafanikio nchini Iraq.

Marekani kwa sasa inawanajeshi wapatao laki moja na 60, 000 nchini Iraq.

Lakini ripoti ya jenerali huyo imeacha baadhi ya masuala nyeti bila ya kujibiwa kama vile kipindi cha muda ambao ameuomba utachukua muda gani na vilevile ikiwa vikosi vya Marekani idadi yao itabaki laki moja na elfu 40 kiwango cha mwanzo kabla ya kuongezwa kwa wanajeshi wa ziada.