1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya Maadili ya CUF yakana kumuhukumu Mbunge Rashid

28 Desemba 2011

Mgogoro ndani cha Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kufukuta, huku leo (28.12.2011)Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuendelea kuwahoji baadhi ya viongozi wa chama wanaotuhumiwa kukiuka katiba ya chama.

https://p.dw.com/p/13ah6
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.Picha: Mohammed Khelef

Hii imekuja baada ya hapo jana, mmoja wa watuhumiwa hao, mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed, kuitwa mbele ya Kamati hiyo, ambayo baadaye aliripotiwa akisema anakataa kuitambua uhalali wake. Amina Abubakar amezungumza na Mkuu wa Idara ya Nidhamu na Maadili ya Kamati hiyo, Abdul Kambaya, juu ya kilichotokea na kitakachotokea hapo baadaye.

Mahojiano: Amina Abubakar/Abdul Kambaya
Mhariri Othman Miraji