1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ataka Ujerumani ionyeshe ubinadamu kwa wakimbizi duniani

26 Februari 2016

Mbunge wa chama Social Demokratik Baerbel Kofler ameteuliwa kuwa Kamishna mpya wa haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani. Bibi Kofler anachukua nafasi ya Christoph Straesser aliejiuzulu jumatatu iliyopita

https://p.dw.com/p/1I1bE
Kamishna mpya wa haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani Baebel Kofler
Kamishna mpya wa haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani Baebel KoflerPicha: DW/T. Shahzad

Baraza za mawaziri la Ujerumani lilimteua mbunge huyo kutoka jimbo la Bavaria kuushika wadhifa huo kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Berlin. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 48 ni mwanachama wa chama cha Social Demokratik kilichomo katika serikali ya mseto.

Kamishna huyo mpya wa haki za binadami ni mjumbe wa kamati ya Bunge inayoshughukilia ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo na pia yumo katika kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya nchi za nje.

Kamishna wa hapo awali Christoph Straesser aliejiuzulu alisema katika mahojiano kwamba aliuchukua uamuzi huo baada ya sheria za kuomba hifadhi ya ukimbizi kufanywa ngumu zaidi nchini Ujerumani.

Kamishna mpya, Baerbel Kofler amesema kutimiza wajibu wa kibinadamu ndiyo msingi wa kila kitu. Anakusudia kuchukua hatua ili Ujerumani ionyeshe wajihi wa kibinadamu katika kushuhgulikia dhiki za wakimbizi duniani.

Mwanasiasa huyo anachukua wadhifa huo katika kipindi kigumu kutokana na mgogoro mkubwa wa wakimbizi. Ujerumani imeshawapokea wakimbizi zaidi ya Milioni moja mnamo kipindi kifupi. Mgogoro huo pia umesababisha magawanyiko miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.

Wapinzani wa wakimbizi waongezeka nchini

Nchini Ujerumani upinzani dhidi ya wakimbizi unaongezeka.Japo idadi ya wanaowapinga wakimbizi ni ndogo,wasi wasi unaongezeka juu ya upinzani huo. Baadhi ya nyumba za kuwahifadhia wakimbizi zimeshambuliwa.

Wakimbizi nchini Ujerumani
Wakimbizi nchini Ujerumani

Baerbel Kofler aliingia katika Bunge la Ujerumani mnamo mwaka wa 2004. Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa mwenyewe, yeye pia ni mjumbe wa jumuiya ya wafanyakazi ya IG Metall.

Amesema anatambua kwamba jukumu analochukua ni kubwa Ameeleza kuwa Ni jukumu linalohitaji uwajibikaji mkubwa. Majukumu yameongezeka katika miaka iliyopita hivi karibuni. Majukumu na maswali yataongezeka juu misaada ya kibinadamu." Kamishna huyo mpya wa masuala ya haki za binadamu wa serikali ya Ujerumani bibi Baerbel Kofler amesema siyo Syria na nchi jirani zinazokabiliwa na changamoto kubwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amemsifu Kamishna huyo mpya kuwa mtu mwenye uwezo wa kuzikabili changamoto.

Kofler alizaliwa katika mji wa Freilassing,katika jimbo la Bavaria, na alifanya kazi Benki baada ya kumaliza masomo. Mnamo mwaka wa 1987 alifanya masomo tekinolojia ya habari na mawasiliano kwa njia ya mtandao

Pia alifanya masomo ya lugha za kirusi na kihispaniola kwenye Chuo kikuu cha Salzburg. Mnamo mwaka wa 1999 alienda kuwa mhadhiri kwenye chuo kikuu cha ufundi mjini Moscow.

Mwandishi: Abdul Mtullya, afp/ZA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman