1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Homa ya uti wa mgongo imesababisha vifo Uganda

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOk

Nchini Uganda,mripuko wa homa ya uti wa mgongo na ubongo,umeua si chini ya watu 110 katika kipindi cha kama miezi miwili wakati mipango ya kuzidisha chanjo dhidi ya ugonjwa huo ikiimarishwa.Maafisa wa siha wamesema,kuna uwezekano kuwa watu zaidi wamepoteza maisha yao kaskazini mwa nchi katika yale maeneo ya ndani ya umasikini na mapigano, tangu ugonjwa huo kuripotiwa mwanzoni mwa mwaka. Homa hiyo ambayo huambukizwa kwa chafya na kikohozi,mara nyingi husababisha kifo.