1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Mafuriko yasababisha hasara kusini mwa Sahara

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPN

Mvua kubwa na mafuriko yameteketeza mazao na miundombinu katika nchi kama nchi 17 za Kiafrika, kusini mwa Sahara.Inatathminiwa kuwa,kuanzia Senegal hadi Ethiopia,kiasi ya watu milioni 1 wameathirika.Kwa mujibu wa msemaji wa kituo cha misaada ya dharura nchini Ghana,baadhi ya vijiji vimetoweka kabisa.

Uganda na Ethiopia,maelfu ya watu wamelazimika kuondoka makwao kwa sababu ya mafuriko.Mashirika ya misaada yameonya kuwa maeneo yaliyofurika sasa yanakabiliwa na hatari ya kutokea magonjwa yanayosababishwa na maji machafu kama vile kipindupindu.

Vile vile kuna upungufu wa chakula na dawa katika maeneo hayo.Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema,huenda kukatokea uvamizi mkubwa wa nzige kwa sababu ya mafuriko hayo.