1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Marekani kusaidia kufyeka waasi wa LRA

6 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSQ

Marekani yumkini ikasaidia juhudi za kanda kuwakamata waasi wa Uganda ambao wameendesha uasi wa kikatili uliodumu kwa miaka 20 kaskazini mwa Uganda iwapo mazungumzo ya kukomesha mzozo huyo yatashindwa.

Msaidizi waziri wa mambo ya nje wa Marekani kwa masuala ya Afrika Jendayi Frazer amesema wanahisi wana sababu ya msingi chini ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusaidia kuwafagia waasi wa LRA.Amewaambia waandishi wa habari kwamba kwa waasi mazungumzo ya amani ni njia ya kujikwamuwa na njia nyengine ni kuimarisha juhudi za kuwakamata na kwamba kwa hakika watasaidia juhudi hizo.

Wawakilishi wa serikali ya Uganda na waasi wa LRA wamekuwa katika mazungumzo ya amani nchini Sudan tokea mwezi wa Julai mwaka 2006.Mazungumzo hayo yamekuwa yakiburuza miguu ambapo wawakilishi wa waasi wamekuwa wakihoji kujifunga kwa serikali kwa mazungumzo ya awali yaliokubaliwa na pande hizo mbili.

Waasi hao pia wamekuwa wakitilia mashaka iwapo msuluhishi serikali ya ndani ya Sudan ya Kusini haina upendeleo katika dhima yake hiyo.