1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Museveni aunga mkono makubaliano na Ulaya

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlo

Rais Yoweri Museveni wa Uganda hapo jana ameunga mkono makubalino ya muda ya biashara yaliofikiwa kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya kuchukuwa nafasi ya makubaliano nafuu ya ushuru yanayomalizika mwaka huu.

Museveni ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Kampala kwamba haoni haja ya kuhofia kufanya biashara na Ulaya na kwamba anakubaliana na Umoja wa Ulaya kuwa mazungumzo hayo ya biashara hayapaswi kuendelea bila ya kuwa na mwisho.

Amesema anaitaka Jumuiya ya Afrika Mashariki kusaini makubaliano hayo kama kundi na kwamba amekuwa na mawasiliano na wanachama wengine wa jumuiya hiyo ya nchi tano.