1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA.Bunge laidhinisha kikosi cha kulinda amani kipelekwe nchini Somalia

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSW

Bunge la Uganda limepitisha mswaada wa kuwapeleka wanajeshi wake kujiunga na kikosi cha umoja wa nchi za Afrika cha kulinda amani nchini Somalia.

Naibu wa waziri wa ulinzi wa Uganda Ruth Nankabirwa amesema kuwa nchi yake iko tayari kuwapeleka wanajeshi wake nchini Somalia ila kinachosubiriwa ni mipango ya kuwasafirisha kwa ndege wanajeshi hao kutoka kwa serikali ya Algeria.

Uganda itapeleka kikosi chake cha wanajeshi 1500 kama mchango wake katika kuunda kikosi cha wanajeshi wa umoja wa Afrika watakao linda amani nchini Somalia.

Hata hivyo umoja wa Afrika mpaka sasa umefanikiwa kupata nusu tu ya idadi ya wanajeshi 8000 wanaohitajika.

Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Ali Mohamed Gedi ameitaka jamii ya kimataifa itie mkazo ili kikosi cha kulinda amani kipelekwe nchini mwake.