1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Jeshi la Uganda laimarisha doria mpakani na Kongo

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaS

Jeshi la Uganda linaimarisha doria katika eneo linalopakana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya wapiganaji wanaoaminika kuwa waasi kushambulia kijiji kimoja siku ya jumatano na kupora maduka.watu watatu waliuawa katika shambulio hilo.

Kwa mujibu wa maafisa wa kijeshi wapiganaji hao wanaaminika kuwa waasi wa Kongo au wapiganaji wa zamani waliokataa kurejea katika maisha ya kawaida.Wapiganaji hao walishambulia kituo cha Rutogota ulio magharibi mwa mkoa wa Kanungu kabla kuvuka mpaka.