1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Mifuko ya plastiki yapigwa marufuku

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmd

Serikali ya Uganda inapiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki ili kupunguza mrundiko wa taka mjini humo unaoathiri huduma za maji.Badala yake wananchi wanaagizwa kutumia majani ya migomba yaliyotumika kitamaduni ili kubebea bidhaa zao.

Agizo hilo linatolewa baada ya visiwa vya Zanzibar kuchukua hatua hiyo mwaka jana.Nchi za Kenya na Tanzania Bara zinapanga kuongeza kodi ya mifuko ya plastiki inayochafua mazingira.

Kwa mujibu wa wanamazingira mifuko hiyo hukusanyika kandokando ya barabara na maeneo yasiyotumika na kuathiri mazingira na wanayama.Kwa upande mwingine ndege aina ya Marabou yaani Kongoti wanahitaji mifuko hiyo kwa chakula.

Katika sheria hiyo mpya makampuni yanapigwa marufuku kuzalisha,kununua au kutumia mifuko ya plastiki.