1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Shirika la kutetea haki za binadamu HRW lalaumu sheria za ulawiti

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWV

Shirika la Kutetea haki za binadamu Human Rights Watch linalaumu serikali ya Rais Yoweri Museveni kwa kupigia debe sheria inayopinga ulawiti.Kauli ya shirika hilo inachochea moto mjadala nchini humo ambako wasenge na wasagaji wanadai haki zao na kutambulia katika jamii.Makundi ya kanisa yanapinga hatua hiyo.

Usenge haukubaliki katika jamii nyingi barani Afrika jambo linalosababisha wahusika kufanya shughuli hizo kwa siri ili kuepuka kubaguliwa.

Shirika la Kutetea haki za binadamu Human Rights Watch lilimuandikia waraka Rais Museveni na kutoa wito wa kufanywa mabadiliko ya kisheria ili kumaliza ubaguzi wa wasenge.

Suala hilo lilijotokeza mapema mwezi huu pale kundi moja la kutetea haki za wasenge lilipofanya mkutano na waandishi wa habari ili kudai kutambuliwa katika jamii.

Hatahivyo wengi wao waligubika nyuso zao.Mkutano huo uliyachagiza makundi ya kanisa kuandamana mjini Kampala kupinga hatua hiyo.

Kwa mujibu wa wanaharakati nchi ya Uganda ina wasenge takriban nusu milioni huku idadi kamili ya wakazi wake ikiwa milioni 31.