1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Waziri wa afya wa zamani mahakamani kwa ubadhirifu

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhx

Waziri wa afya wa zamani nchini Uganda Jim Muhwezi alifikishwa mahakamaji hapo jana kwa mashtaka ya ubadhirifu.

Waziri huyo wa zamani na manaibu wake wawili Mike Mukula na Alex Kamugisha pamoja na msaidizi mmoja wa Rais Museveni Bi Alice Kaboyo wanashtakiwa kwa kuiba dola milioni 1.63 zilizotengwa mahsusi kwa kununulia chanjo za watoto na dawa za Ukimwi.

Maafisa hao wa wazamani katika wizara ya afya aidha wanadaiwa kuhusika na kashfa ya kuiba pesa kutoka Mfuko wa Fedha duniani Global Fund za kupambana na Ukimwi ,Kifua Kikuu na Malaria.Kashfa hiyo ilisababisha taasisi hiyo kuzuia mamilioni ya dola za usaidizi mwaka 2005.Kesi hiyo inasikizwa tena Oktoba 29.