1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeini za urais Marekani zakaribia ukingoni

Kalyango Siraj3 Novemba 2008

Obama anaongoza kura za maoni McCain asema yu ngangari

https://p.dw.com/p/FmYK
Sen. Barack Obama, akiwapungia mkono waliokuwa wanamsikiliza katika chuo kikuu cha Cincinnati Cincinnati, Ohio Jumapili, Nov. 2, 2008Picha: AP

Leo jumatatu ni siku ya mwisho ya kutafuta kura nchini Marekani kwa wagombea wawili wa kiti cha urais nchini humo,Barack Obama wa chama cha Democratc na mwenzake John McCain wa chama cha Republican.Hata hivyo utafiti mpya wa maoni uliotolewa leo jumatatu unaonyesha kama Obama anaongoza.

Kampeini za mwisho mwisho zimemulika majimbo ambayo kawaida ni ya warepublican yanaonekana yanampendelea mgombea wa chama cha Democratic.

Na kwa upande mwingine maoni hadi sasa yanamuonyesha Barack Obama kama anaelekea kuvunja daftari ya kihistoria ya masuala ya kisaisa ya Marekani.Utafiti wa maoni ya wananchi unaonyesha kuwa yuko mbele ya mpinzani wake.Maoni ambayo yamechapishwa na Gallop-USA Today yanaonyesha kama Obama yuko mbele na alama 11 mbele ya McCain akiwa na asili mia 55 dhidi ya asili mia 44 ya McCain.

Utafiti wa mwingine ambao umefanywa kwa ushirikiano wa jarida la Wall Street Journal na NBC News unaonyesha Obama akiwa mbele na asili mia 53 huku mwenzake akiwa na asili mia 43. Tena katika utafiti wa shirika la CNN,Obama asili mia 53 na McCain 46.Maoni mapya ya gazeti la Washington Post na ABC News yanaonyesha kama Obama alipata asili mia 54 na 43 ya McCain.

Pia Obama anaongoza katika majimbo yenye ushindani mkubwa,ambapo kila upande aidha ushinde ama upoteze.

Wakati akihutubia mkutano mmoja McCain ambae anasema kuwa hatishingishiki na maoni hayo na kudai kuwa anaamini atashinda.Akiwa New Hampshire seneta McCain amemlaumu Obama kuhusu msimamo wake kuelekea kodi akisema kuwa anapanga kupandisha kodi‚kupandisha viwango vya kodi kunaufanya uchumi ambao si mzuri kuzidi kuharibika zaidi.Na kupunguza viwango cha kodi kunasaidia kuunda ajira,kunakusaidia kuwa na pesa mfukoni na pia kuimarisha uchumi wetu. Ikiwa nitachaguliwa kama rais sita tumia dola zenu zaidi ya trillioni.Seneta Obama atafanya hivyo.na hawezi hatafanya hivyo bila kupandisha viwango vya kodi zenu na hivyo kutulimbikia madeni zaidi’McCain amesema.

McCain,pamoja na mpinzani wake leo watakuwa na kibarua cha kuchanja mbuga za mikoa saba ili kujipigia debe. Yeye Obama katika mkutano wa jana mjini Ohio nae alimumwagia mbovu mwenzake McCain, akisema sera zake zitakuwa za kuendeleza enzi ya rais George W. Bush ya mgogoro wa kiuchumi pamoja vita visivyoisha vya Iraq huku akipuuza hali ya Afghanistan,

‚Wakati kama huu kitu ambacho hatuwezi kuvumilia tena kwa kipindi kingine cha miaka minne ni nadharia za kiuchumi ambazo ni zilezile moja za zamani na ambazo hazifai kwa kuwa zimepitwa na wakati.Zinazosema kuwa ni lazima tutoe zaidi pesa zetu na kuwapa mamilionere na mabilionere na makampuni makubwamakubwa na kufikiri kuwa utajiri unamtirirkia kila mtu.’ amesema Obama.

Obama akiwa anakaribia kuvunja daftari za historia ya Marekani ya kuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwa rais wa nchi hiyo, huku mwenzake McCain akisisitiza kuwa atafanya miujiza na kushinda mpambano huo.

Tayari wamarekani millioni 20 wamepiga kura zao katika mfumo wa kura za mwanzo.