1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za uchaguzi wa rais zadhaminiwa kwa rushwa Kenya

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cd0Z

NAIROBI

Wagombea urais nchini Kenya wamechangisha takriban fedha zao zote katika kampeni za uchaguzi katika miezi ya hivi karibuni kwa njia ya hujuma na kulazimisha watu kulipa kwa kutumia vitisho.

Kwa mujibu wa repoti ya Muungano wa Kugharimia Michango ya Kisiasa Kiuwajibikaji Rais Mwai Kibaki na wapinzani wake wakuu Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wamegarimia asilimia 60 ya kampeni yao kuanzia tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 15 mwezi wa Desemba kwa njia ya rushwa.

Charles Otieno aliyeongoza utafiti wa repoti hiyo iliodhaminiwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa amesema wamegunduwa kwamba baadhi ya wafanyabiashara wamelazimishwa kulipa fedha.

Uchaguzi mkuu wa Kenya umepangwa kufanyika hapo tarehe 27 mwezi wa Desemba.