1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni zafikia mwisho kabla ya uchaguzi.

25 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfzg

Nairobi. Kampeni za uchaguzi mkuu wa rais nchini Kenya ambao wagombea wana nafasi sawa zimekamilika jana Jumatatu huku wagombea wanaoongoza wakifanya juhudi za mwisho za kupata kura, wakati polisi wameripoti matukio ya hapa na pale ya ghasia katika mikutano ya hadhara nchini humo.

Rais Mwai Kibaki pamoja na mpinzani wake wa karibu , kiongozi wa upinzani Raila Odinga , wamewataka wapiga kura kuwaamini na kuwapa kura hapo siku ya Alhamis.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga , ambaye amekuwa akiongoza katika kura ya maoni ya wapiga kura , amerudia madai yake kuwa serikali inapanga kuiba kura.

Polisi wamefyatua mabomu ya kutoa machozi na kuwatawanya watu waliokuwa wakileta ghasia kati ya wafuasi mahasimu wa wagombea hao katikati ya jiji la Nairobi baada ya mikutano kumalizika. Ghasia hizo zilidhibitisha haraka , na kuondosha hofu kuwa kutakuwa na machafuko kabla ya uchaguzi kutokana na uhasama wa kikabila pamoja na madai ya rushwa.