1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni zakaribia kumalizika Ujerumani

21 Septemba 2013

Kansela Angela Merkel na mpinzani wake mkubwa wamekuwa wakizunguka nchi nzima ya Ujerumani katika siku za mwisho za kampeni, wakiwaomba Wajerumani kura katika uchaguzi unaonekana kutotabirika Jumapili(22.09.2013)

https://p.dw.com/p/19lQc
ARCHIV - Wahlplakate verschiedener Parteien stehen am 15.08.2013 in Stuttgart (Baden-Württemberg) an einer Straße. Foto: Foto: Franziska Kraufmann/dpa (Zu lsw Korr: «Bundestagswahl am Sonntag als erster Stimmungstest für Grün-Rot» vom 20.09.2013) +++(c) dpa - Bildfunk+++ ***FREI FÜR SOCIAL MEDIA***
Mabango ya vyama vya SPD , kijani , Die Linke na FDPPicha: picture-alliance/dpa

Wakikamilisha uchaguzi ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa tu ni wa haiba lakini ukikosa mada muhimu , Merkel na mpinzani wake kutoka chama cha Social Democratic SPD, Peer Steinbrück , pia amepanga mikutano ya dakika za mwisho leo Jumamosi(21.09.2013) kabla ya kila kitu kutulia na kuwaachia wapiga kura kuamua.

Kansela kutoka chama cha Christian Democratic CDU ameshughulika na makundi ya wapiga kura siku ya Ijumaa katikati ya mji wa kaskazini mwa Ujerumani wa Hannover.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) ist am 18.09.2013 auf dem Alten Garten in Schwerin (Mecklenburg-Vorpommern) bei einer Wahlkampfveranstaltung der CDU zur Bundestagswahl zu sehen. Am 22. September 2013 wird in Deutschland ein neuer Bundestag gewählt. Foto: Jens Büttner/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kansela Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Alikuwa anatarajiwa leo kusafiri kwenda katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujerumani kwa ajili ya mkutano mwingine wa kampeni mjini Munich ikiwa ni saa tatu tu baadaye. Wapiga kura wa Bavaria Jumapili iliyopita walimpa ushindi wa kishindo kansela merkel katika uchaguzi wa jimbo.

Steinbrück, ambaye ameingiza ucheshi wake pamoja na malalamiko kuhusu Merkel katikati ya kampeni yake , alikuwa akihutubia kundi la wapiga kura jana Ijumaa(20.09.2013) katika miji ya kati ya Wiesbaden, Marburg na Kassel.

Uchunguzi wa maoni

Uchunguzi mpya wa maoni ya wapiga kura yanatabiri kuwa hadi dakika ya mwisho hakuna mshindi wa moja kwa moja kati ya muungano unaoongozwa na Merkel pamoja na vyama vitatu vya upinzani .

Stand: 12.09.2013 --- DW-Grafik: Peter Steinmetz
Utabiri wa maoni katika uchaguzi wa Jumapili

Merkel ambaye chama chake cha Christian democratic CDU pamoja na chama ndugu cha CSU vinatarajiwa kupata asilimia karibu ya 40, huenda vikahitaji kumpata mshirika mpya baada ya uchaguzi iwapo havitapata wingi katika bunge pamoja na chama kishiriki katika serikali ya sasa cha FDP.

Maoni ya wapiga kura yaliyochukuliwa na kituo cha televisheni cha RTL, yanaonesha kuwa chama cha FDP huenda kikazuiwa kuingia katika bunge jipya chini ya sheria inayopiga marufuku vyama vidogo vilivyopata chini ya asilimia 5 ya wabunge.

Uwezekano mbadala kwa Merkel unakiweka katika hali ya mkwamo chama cha Social Democratic ambacho kinatarajiwa kupata asilimia 26 ya kura kwa mujibu wa maoni yaliyokusanywa na taasisi ya Forsa na chama cha kijani ambacho kinatabiriwa kupata asilimia 10. Hakuna chama miongoni mwa vyama vinne vikuu ambacho kiko tayari kufanya muungano na chama cha tano cha Die Linke ambacho kinatabiriwa kupata asilimia 9 ya kura.

Wahlarena 2013 am 11.09.2013 im Kunstwerk in Mönchengladbach Der Kanzlerkandidat Peer Steinbrück ( SPD ) Foto: Revierfoto
Mgombea wa chama cha SPD Peer SteinbrückPicha: picture-alliance/dpa

FDP mashakani

Kansela , ambaye amekuwa akifanya kampeni yake kama mzalendo halisi , akiwataka Wajerumani kuendelea kubaki na utaratibu ambao umeleta mafanikio na kutomtaja kabisa Steinbruck , amesema anataka kuendelea na muungano wake wa sasa katika serikali pamoja na chama kidogo kinachopendelea wafanyabiashara cha Free Democrats, FDP.

Amekuwa akitoa maelezo yasiyoeleweka kwa wito wa FDP wa kutaka kupata kura za mbinu. FDP kinawaelekeza wapiga kura kuwa picha kura kwa chama cha FDP ili Merkel achaguliwe.

Bundesgesundheitsminister Philipp Rösler (FDP) spricht am Sonntag (23.01.2011) in Potsdam auf dem Neujahrsempfang der Brandenburger FDP. Foto: Bernd Settnik dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mwenyekiti wa chama cha FDP Philipp RöslerPicha: dapd

Chama cha Christian Social Union CSU cha jimbo la Bavaria chama ndugu na chama cha kansela Merkel cha CDU, kimezipuuza juhudi za chama cha FDP kupora kura za CDU na CSU.

"Ningewashauri wote sisi kutovutana kuhusu kura, lakini tupambane na wapizani wetu wa kisiasa, amesema waziri mkuu wa jimbo la Bavaria na kiongozi wa chama cha CSU katika gazeti la Die Welt.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe

Mhariri: Sudi Mnette