1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanali wa zamani wa Kijeshi Theoneste Bagosora ahukumiwa kifungo cha maisha kwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda

18 Desemba 2008

Mahakama ya uhalifu wa kivita kwa ajili ya Rwanda ICTR iliyo mjini Arusha imemhukumu kifungo cha maisha kanali wa kijeshi wa zamani Theoneste Bagosora kwa mauaji ya halaiki yaliyofanyika mwaka 1994 nchini Rwanda.

https://p.dw.com/p/GJEA
Kanali Theoneste Bagosora ahukumiwa kifungo cha maishaPicha: AP

Yapata watu laki nane wanaripotiwa kuuawa kikatili katika kipindi cha siku 100.

Bagosora anakabiliwa na mashtaka 11 ya uhalifu wa kivita,mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mwandishi wetu wa Arusha Nikodemus Ikonko alikuwako mahakamani na ametuandalia taarifa ifuatayo.