1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanisa na Siasa - waonavyo Wajerumani wa Mashariki

Samia Othman3 Novemba 2009

Wajerumani wa Mashariki waingia katika Siasa kupitia Kanisa

https://p.dw.com/p/KIKJ
Christoph Matschie alikuwa mchungaji na sasa ni Mwenyekiti wa SPD wa jimbo la ThüringiaPicha: picture-alliance/ ZB

Yeyote anaetaka kuangalia wasifu wa wanasiasa kutoka Ujerumani ya mashariki, ni lazima kuangalia ni wanasiasa wangapi kutoka vyama vya CDU, SPD ama hata kile cha ulinzi wa mazingira cha kijani ambao wamesomea masuala ya elimu ya dini, watoto waliokulia katika utaratibu wa kikanisa wanajishughulisha zaidi kama walivyo makasisi.

Ripoti ya Hilde Weeg inayoangalia vipi wanasiasa kutoka upande wa mashariki ya Ujerumani walivyoingia katika siasa kupitia katika kanisa.

Mwishoni mwa mwaka 1989 walikuwamo miongoni mwa wengi waliokuwamo katika mikono ya kanisa na wakaandamana hadharani na kutokana na harakati hizo za kutaka kupatikana kwa jamii mpya wakajitokeza kuwa wanasiasa. Kwa mfano mwanasiasa mwandamizi wa SPD Christoph Matschie, waziri mkuu aliyeko madarakani katika jimbo la Thüringer kutoka chama cha CDU Dieter Althaus na makamu spika wa bunge la Ujerumani Katrin Göring-Eckardt kutoka chama cha walinzi wa mazingira The Greens.

O-Ton Katrin Eckardt

"Nimepata kuwa mwanasiasa kupitia kundi la vijana wa kanisa, wakati huo katika mji wa Gotha, hapo ndipo nilipokulia, lakini wakati huo huo tulikuwa tunajadili pia masuala ya kisiasa. Tunaishi vipi katika Ujerumani mashariki, hali ikoje katika mfumo wa ikolojia, tunafikiri nini kuhusu haki ya uchumi wa dunia, maswali yote haya tuliyajadiliwa wakati ule."

Katrin Göring-Eckardt, amezaliwa mwaka 1966 ambapo baba na mama yake walikuwa waalimu wa kucheza muziki. Hii leo ni mmoja kati ya wanasiasa wa ngazi ya juu wa Ujerumani katika chama cha kijani na pia ni mwenyekiti wa sinodi ya kanisa la Kiprotestanti nchini Ujerumani. Hakujikuta tu katika miaka ya 80 kuwa katika kundi la kanisa, lakini pia alijipatia uzoefu wa mfumo wa kidemokrasia.

O-Ton Katrin Göring

"Ilikuwa ni mahali pekee, ambapo mtu anaweza kujadili kwa uhuru na mahali ambapo mtu anaweza kujifunza, kubadilishana mawazo, na kanisa lilikuwa limejenga mfumo wa kidemokrasia, ndani ya udikteta wa serikali ya Ujerumani mashariki, DDR, lakini hilo pia lilikuwa moja katika ya masuala yaliyotushughulisha katika demokrasia, ambapo wengine hawakuweza kujifunza."

Ni wanasiasa wangapi wa Ujerumani mashariki wengine ambao hawakupata uzoefu kupitia katika kanisa ambao hawakuingia katika siasa. Katika Ujerumani mashariki kuhusika katika kanisa kulikuwa na maana ya kuipinga serikali na pia kufuatiwa na matokeo mabaya. Hali hiyo pia ilimkuta mwenyekiti wa SPD wa jimbo na mkuu wa kundi la wabunge Christoph Matschie. Baba yake alikuwa mchungaji, na hii ilitosha kwa familia nzima kutengwa. Matschie hakuruhusiwa kusomea udaktari, kama njia mbadala , alichagua kama wengine walivyofanya kujifunza elimu ya dini, na Oktoba mwaka 1989 alikuwa mwanachama wa kile kilichokuja baadaye kuitwa SDP na kuwa mmoja wa waasisi wa iliyojulikana kama meza ya duara mjini Berlin. Pamoja na wanasiasa hao pia kuna waziri mkuu Dieter Althaus, ambaye amepata kujiimarisha kupitia eneo lake alikozaliwa la Eischsfeld ambalo ni eneo la Wakatoliki la Thüringia ya kaskazini. Baba yake ni mmoja wa waanzilishi wa CDU ya upande wa mashariki. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 51 mwaka huu ulikuwa mbaya kwake kutokana na ajali aliyopata wakati akifanya mchezo wa kuteleza katika barafu na hali yake ya baadaye ya kisiasa haifahamiki, na hii inamaana ya yeye binafsi kulirudia kanisa zaidi. Hata kwa wanasiasa wengine kanisa lina nafasi na jukumu kama hilo.

Mwandishi Hilde Weeg/ ZR / Sekione Kitojo

Mhariri Saumu Mwasimba.