KANSAS:Watatu wauwawa katika mashambulizi ya risasi
30 Aprili 2007Matangazo
Watu watatu wameuwawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mashambulizi ya risasi kwenye eneo la biashara mjini Kansas katika jimbo la Missouri,Marekani.
Mtu aliyekuwa na bunduki aliingia kwenye duka kubwa la biashara na kuanza kufyetua risasi na kuua watu wawili katika duka hilo lililokuwa na msongamano mkubwa wa watu na kuwajeruhi wengine wawili. Mshambuliaji huyo baadaye alikutikana amekufa lakini haijajulikana ikiwa alijiua au aliuwawa na polisi kwa kupigwa risasi.