1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani awasili Urusi.

17 Mei 2007

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kama rais wa baraza la Umoja wa Ulaya leo yupo Urusi kufanya mazungumzo na rais Vladmir Putin katika juhudi za kufikia mkataba mpya wa ushirikiano baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya wakati ambapo pande mbili hizo zimezidi kufarakana katika uhusiano wao.

https://p.dw.com/p/CHEB
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais Putin wa Urusi
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais Putin wa UrusiPicha: AP

Utatanishi uliopo katika uhusiano baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya unatokana na hatua ya Urusi kupiga marufuku nyama kutoka Poland kuingizwa nchini Urusi.

Urusi pia inazozana na Estonia ambae ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya kutokana na mkasa uliosababishwa na kuhamishwa kwa sanamu ya askari wa kisoviet inayokumbusha juu ya vita kuu vya pili.

Mazungumzo hayo yanahudhuriwa pia na rais wa tume ya Umoja wa Ulaya bwana Barosso.

Mazungumzo juu ya kurefusha mkataba wa ushirikiano wa miaka kumi iliyopita yalianza kufanyika kwenye mkutano mkuu wa mjini Helsinki. Lakini wakati huo pia mazungumzo hayo tayari yalishakwama kutokana na veto ya Poland.

Poland ilitumia veto kilipiza kisasi hatua ya Urusi kupiga marufuku nyama yake kuuzwa nchini Urusi.

Urusi imesema imechukua hatua hiyo kutokana na sababu za kiafya.

Ujerumani kama rais wa sasa wa baraza la Umoja wa Ulaya inafanya juhudi ili hatua ziweze kuchukuliwa katika kuondoa mivutano.

Mkataba wa sasa juu ya ushirikiano baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya unamalizika mwanzoni mwa mwezi wa desemba mwaka huu. Lakini unaweza kurefushwa.

Lakini hayo yatategemea matokeo ya juhudi zinazofanywa sasa katika kuondoa mivutano baina ya pande hizo mbili.

AM