1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel akutana na Dalai Lama licha ya lawama za China

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNM

Berlin:

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anapanga kuzungumza hii leo na mkuu wa kidini wa Tibet Dalai Lama, licha ya lawama kali kutoka serikali ya jamhuri ya umma wa China.Ingawa mazungumzo hayo yatakayofanyika katika ofisi ya kansela mjini Berlin yanatajwa kua ni ya” kibinafsi ya kubalidilishana fikra”,serikali ya mjini Beijing imemtaka pia balozi wa Ujerumani ajieleze.Serikali ya China imeakhirisha mkutano wa ngazi ya juu wa pande mbili pamoja na waziri wa sheria Brigitte Zypries, uliokua ufanyike hii leo mjini München, kwa kile walichokiita “sababu za kiufundi”.Beijing inatishia kuchukua hatua zaidi.China inayoikalia Tibet tangu mwaka 1950 imekua ikilaani aina yoyote ya mazungumzo kati ya wanasiasa wa kigeni na Dalai Lama anaeangaliwa kama kitambulisho cha upinzani dhidi ya kukaliwa Tibet.