1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

110112 Monti Berlin

Mohammed Khelef11 Januari 2012

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anakutana na Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti, mjini Berlin, kujadiliana masuala kadhaa ya mahusiano baina ya nchi zao, hasa tatizo la madeni katika kanda ya euro na uchumi wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/13hLQ
Angela Merkel, Nicolas Sarkozy na Mario Monti
Angela Merkel, Nicolas Sarkozy na Mario MontiPicha: dapd

Bila ya shaka kuna mengi zaidi yanayopelekea mkutano huu wa leo, hasa la uhusiano binafsi kati ya Italia na Ujerumani, ambao uliingia doa baada ya kuondoka madarakani kwa waziri mkuu wa zamani, Silivio Berlusconi.

Siku kumi kabla ya kujiuzulu kwake, gazeti la familia "Il Giornale", lilisambaza uvumi kwamba Belusconi alimwita Kansela Merkel kama "culona inchiavabile", yaani mtu asiyewezekana. Gazeti likaandika kuwa, kwa sababu ya kauli hiyo, ndiyo maana Kansela Merkel aliyakata mazungumzo ya simu kati yake na Berlusconi na Rais Napolitano wa Italia.

Lakini hata bila ya mkasa huu, ni jambo lisilo siri kwamba mwishoni wa uwaziri mkuu wa Berlusconi, palikuwa na ukungu kwenye mahusiano kati yake na Merkel. Ndiyo sababu Mario Monti amefanya ni jukumu la ofisi yake, kusafisha hewa ya kidiplomasia iliyoanza kuchafuka:

unafahamu sote kwamba tumejengwa vibaya mbele ya uso wa dunia na Ulaya. Tunajuwa kuwa huo ni uongo, lakini pia tuna wajibu wa kuonesha tafauti." Amesema Monti kabla ya kuondoka Rome.

Mario Monti akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mario Monti akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.Picha: dapd

Hii leo Monti anatarajiwa kupiga hatua nzuri katika hilo, ikiwemo ile ya kujitenga kando na upinzani wa mtangulizi wake katika suala la mipango ya kuwa na kodi ya masuala ya fedha, barani Ulaya, ambayo inapigiwa chapuo na Ufaransa na kuungwa mkono na Ujerumani. Monti ameahidi tangu mwanzo kwamba atafanya kazi pamoja na mataifa hayo katika suala hili.

Ni juu ya kufanya kazi huko pamoja, ambapo Merkel na Monti wanatarajiwa kutuwama katika mazungumzo yao ya leo, hasa katika kujenga msingi wa eneo gani kodi hiyo ya masuala ya fedha ichukuliwe, aidha kwenye mataifa wanachama wa sarafu ya euro tu, au kwa mataifa yote 27 ya Umoja wa Ulaya.

Litajadaliwa pia suala la namna ambavyo Italia imejipanga kutekeleza masharti iliyowekewa na Umoja wa Mataifa yanayotumia Sarafu ya Euro na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kuhusiana na nidhamu yake ya kibajeti, na zaidi juu ya mwenyewe Monti alivyojipanga kunyanyua ukuwaji wa uchumi wa nchi yake.

ika hilo Monti anasema kwa kujiamini, kwamba kwanza Italia iko mbali sana na zile siku za kutowajibika. Baada ya machungu ya kukaza mkanda ambayo raia, vyama vya wafanyakazi na wote nchini Italia wamekabiliana nayo, Monti anasema Italia imejenga hisia za kupevuka, na sasa inataka nchi nyengine zijifunze kwao. Na pili, hata Ujerumani pia, kwa hali inayoeleweka, katika mambo ya maingiliano barani Ulaya, katika soko la pamoja la Ulaya na katika sarafu ya euro, nayo itafaidika.

Kansela Angela na Rais Nicolas Sarkozy mjini Berlin.
Kansela Angela na Rais Nicolas Sarkozy mjini Berlin.Picha: Reuters

"Mara moja gazeti la Süddeutsche liliandika kwamba: Waziri Mkuu mpya Mario Monti ni kama mkwe wa kiume wa kizamani, kwa sababu anazungumza kidogo, anajionesha yuko makini anavaa mavazi ya kawaida na hafanyi zogo. Naamini katika macho ya Wajerumani, hayo ndiyo mambo muhimu kuwa nayo." Amesema Monti.

Kwa muonekano wa jumla wa Waziri Mkuu wa Italia, hakuna kitu kinachoweza kuharibika, cha kumfanya Kansela Merkel kutilia shaka. Mario Monti anajiwasilisha mwenyewe kama kiongozi mwenye gambo la mwanasiasa anayejiamini, na mazungumzo ya leo yanatarajiwa kuthibitisha hayo.

Mwandishi: Stefan Troendle/Rom (BR)
Tafsiri: Mohammed Khelef
Mhariri: Josephat Charo