1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani nchini Israel

Kalyango Siraj17 Machi 2008

Ziara ina nia ya kuimarisha uhusiano kati ya Ujerumani na Israel

https://p.dw.com/p/DPmb
Wageni wakipita karibu na ukumbi mkuu wa kituo kipya cha kumbukumbu za mauaji ya halaiki cha Yad Vashem mjini Jerusalem ambako Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ametembeleaPicha: dpa

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel kwa sasa yuko nchini Isreal kwa ziara rasmi ya siku tatu.Ziara yake hii imekuja wakati Israel ikiadhimisha miaka 60 ya kuasisiswa na pia kukiwa na kiwingu cha historia ya Ujerumani kuwa husu Wayahudi,na kutarajiwa kuwa ziara yake hii itaimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Kansela Angela Merkel aliwasili jana nchini Israel.Leo ametembelea kituo cha kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wayahudi cha Yad Vashem.

Bi Merker akiandamana na waziri mkuu wa Israel-Ehud Olmert, mawaziri saba kutoka kila upande walipangiwa kuhudhuria ibada ya kuwakumbuka wayahudi millioni sita waliouawa katika vita vikuu vya pili vya dunia.

Kansela ya Ujerumani Angela Merkel,alipowasili mjini Tel Aviv na akigusia yaliyopita amesem akuwa Berlin ina wajibu maalum kwa kuwepo kwa Israel.

Yeye waziri mkuu Olmert,kwa upande wake ameielezea Ujeruamni,miaka 63 baada ya mauaji ya halaiki,kama mshirika mkubwa wa Israel.

Rais wa Israel,Shimon Perez,anasema kuwa Bi Merkel amekuwa bega kwa bega nao wakati huu mgumu.

Mawaziri kwa upande wao,wanatazamiwa kufanya kikao cha pamoja cha kihistoria.Kikao hicho ndicho kitakuwa cha kwanza kwa serikali hizo mbili kufanya kikao cha pamoja cha ushauri.Pia ndio kikao cha kwanza kwa serikali ya Ujerumani kufanya kikao cha pamoja katika ngazi hiyo kwa serikali nyingine nje ya bara la Ulaya.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Israel,Tzipi Livni nae alitarajiwa kufanya mkutano tofauti na mwenzake wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier.Mazungumzo yao yatajikita katika tisho la nuklia kutoka Iran.Mkutano mwingine utakuwa kati ya mawaziri wanaohusika na mambo ya Ulinzi,wa Isreal,Ehud Barak na Franz Josef Jung wa Ujerumani.

Siku ya Jumapili Bi Angela Merkel alisema kuwa ziara yake itasaidia kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Wakati wa mikutano kadhaa na serikali hizo mbili mapatano kadhaa itatiwa saini itakayohusu miradi mbalimbali mkiwemo ya uhifadhi wa mazingira pamoja na ulinzi.

Kansela Merkel alisema kuwa Ujerumani daima haita sahau uwajibikaji wa kihistoria,hatua iliokuwa inamanisha kuwa anagusia mauaji ya halaiki ya wayahudi yaliyofanya na watawala wa Kinazi.

Mwenyekiti wa chama cha Israel cha Meretz cha mrengo wa kushoto, Shulamit Aloni amesema kuwa licha ya historia mbovu ya wajerumani, lakini uhusiano kati ya Ujerumani na Israel ni mzuri.

Kansela wa Ujerumani Merkel amesema jambo muhimu sasa sio kusahau yaliyopita lakini pia la muhimu zaidi ni kuangalia mbele.

Miongoni mwa mada zingine zitakazojadiliwa katika ziara ya Bi Merkel ya siku tatu ni masuala tatanishi kama vile, tangazo la Isreal kuwa inapanga kuanza tena ujenzi wa makazi mashariki mwa Jerusalem pamoja na kuendelea kwa biashara kati ya Ujerumani na adui mkubwa wa Israel ambae ni Iran.