1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani ziarani Urusi

8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DL09

MOSCOW:

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anakutana na rais mteule wa Urusi Dmitri Medwedew mjini Moscow leo hii.Merkel ni kiongozi wa kwanza wa serikali ya kigeni kupokewa na Medwedew,hatua inayotazamwa na Berlin kama ni ishara ya ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.Wakati wa ziara hiyo,Merkel anatazamia kujiarifu zaidi juu ya mipango ya mageuzi iliyotangazwa na Medwedew kuimarisha utawala wa kisheria na kurekebisha uchumi kuwa wa kisasa.Kansela Merkel vvile vile atakutana na Rais Vladimir Putin.Viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili suala la Kosovo na mgogoro wa Iran unaohusika na mradi wake wa nyuklia.